Back to top

Polisi kuwasaka watekaji wanaodai dhahabu na fedha Tarime.

16 November 2019
Share

Jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime Rorya limesema linaendelea kufanya uchunguzi wa vitendo vya utekaji wa watu ambavyo vimekuwa vikitokea katika maeneo mbalimbali huku watekaji wakilazimisha kupatiwa pesa pamoja na mawe ya dhahabu ili kuwaachia mateka.

Akizungumza na ITV kamanda wa mkoa wa kipolisi wa Tarime Rorya Henry Mwaibambe amesema kuwa vimekuwepo vitendo vya utekaji watu,huku watekaji hao wakidai kupatiwa fedha,vitendo ambavyo ameeleza kuwa watahakikisha wanavidhibiti.

Baadhi ya wananchi waliokumbwa na matukio hayo akiwemo mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tarime Bw. Daud Ngicho ambaye alinusurika kutekwa nyara huku mkulima wa alizeti akitekwa nyara kwa kudhaniwa mchimbaji wa madini ya dhahabu.