Back to top

Rais Kenyatta aondoa marufuku ya kutoka nje nyakati za usiku.

20 October 2021
Share

Rais Uhuru Kenyatta ameongoza taifa la Kenya kusherehekea mashujaa waliopigania uhuru wa Kenya.

Katika hotuba yake Rais Kenyatta ametangaza kuondolewa kwa marufuku ya kutoka nje nyakati za usiku iliyowekwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona ambapo amesema amechukua hatua hiyo kutokana na kupungua kwa maambukizi hayo nchini Kenya. 

Aidha Rais Kenyatta amesisitiza kuwa Kenya haitakubali kupoteza sehemu yoyote ya himaya yake kwa taifa lolote,hii ni kufuatia uamuzi wa kesi kuhusu Kenya na Somalia uliotolewa wiki jana na mahakama ya ICJ.


Rais wa Malawi Dkt Lazarus Chawera amekua mgeni maalum kwenye sherehe hizo.