Back to top

Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi wawili .

16 September 2021
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao:- 

(1) Amemteua Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC). Dkt. Kayandabila ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

(2) Mhe. Rais Samia amemteua Dkt. Naomi Bakunzi Katunzi kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kipindi kingine cha miaka mitatu (3).

Uteuzi huu umeanza tarehe 14 Septemba, 2021.