Back to top

Rais wa TLS na Mtego wa Uhalali wa Uchaguzi wa TFF.

11 June 2021
Share

Baada ya Wakili Simoni Patric kupitia kaunti yake ya Instagram kutoa changamoto juu ya uhalali  kuwa Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa TFF Kiomoni Kibamba hana sifa za kuwa Mwanasheria (Legal Qualifications) na haruhusiwi kufanya kazi yoyote ambayo sheria inataka ifanywe na Mwanasheria, na kazi yoyote anayoifanya ni batili kwa mujibu wa sheria namba 341 ya Mwaka 2002 kifungu namba 39 na ni kosa la jinai.

Akimaanisha Mtu mwenye legal qualification maana yake ni Mwanasheria mwenye leseni ya kufanya kazi za kisheria ambayo hutolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania kila mwaka.

Pamoja na TFF kutoa taarifa kupitia akaunti yao instagram kutumia ibara ya 4 (3) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF kuwa  Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wanatakiwa kuwa wanasheia kitaaluma na kuwa mwansheria ni mtu yeyote aliyehitimu shahada ya sheria [LLB].

Wakili Simon Patric alipinga kwa kuandika Tafsiri iliyotolewa na shirikisho kwamba Mwanasheria ni mtu yoyote aliyehitimu shahada ya sheria siyo kweli na inapotosha umma  Kanuni namba 4 imeweka wazi kabisa kwamba Mwenyekiti na Makamu wake lazima wawe ni watu wenye sifa za kufanya kazi ya sheria (Chairman & Vice Chairman shall have legal qualification) na kwakuwa neno lililotumika ni “shall” maana yake ni lazima watu hao wawe na sifa kwa husika, bila hivyo mchakato mzima unaosimamiwa na mtu asiye na sifa ni batili kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi

Tumemtafuta Rais Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) Edward Hosea kupata maoni yake kama yanayodaiwa na Wakili Simon Patric ni kweli Je uchaguzi wa TFF utakuwa batili? Na kuahidi Jumatatu baada ya mapitio ya kina atazungumza rasmi maoni yake juu ya sakata hili.

Tulimtafuta Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi TFF Kiomoni Kibamba hakupokea simu.