Back to top

RAIS WA WAFUGAJI MAMBA ALIWA NA MAMBA

28 May 2023
Share

Luan Nam mwenye umri wa miaka 72, ambaye ni Rais wa chama cha wafugaji wa mamba kaskazini mwa Cambodia, ameuawa baada ya kuteleza na kuanguka ndani ya eneo wanamoishi mamba takriban 40 anaowafuga, wakati akijaribu kuchukua yai la moja ya mamba hao.
.
Watu wa Taifa lililopo kusini-mashariki mwa Bara la Asia, hufuga wanyama hao ili kujipatia mayai, ngozi na nyama. #via #ABC | #picha #AP