Back to top

RC Kigoma:Tumieni vyakula vinavyowazunguka kuboresha afya.

25 October 2021
Share

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Tobias Andengenye ameitaka jamii itumie vyema vyakula vinavyopatikana katika maeneo yanayowazunguka ili kuboresha afya zao kuliko kutumia vyakula vinavyotoka maeneo mengine ambavyo wanadhani ni maendeleo kuvitumia, ili kupambana na utapia mlo kwa watoto.

Ametoa ushauri huo Kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dakta Dorothy  Gwajima, wakati akizindua zoezi la ugawaji wa maziwa lishe kwa watoto, katika maadhimisho ya Wiki  ya Lishe nchini, yaliyofanyika kitaifa mkoani Tabora.

Akiwa katika wodi ya watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete   amesema elimu kuhusu lishe bora inahitajika  ili kuiwezesha jamii kuwa na afya bora.

Akizungumza baada ya kukagua mabanda ya maonesho ya vyakula bora na vyenye virutubisho muhimu, amewataka viongozi wawahamasishe wananchi kuepuka matumizi yasiyo sahihi ya vyakula mbalimbali.

Akitoa salamu za mkoa wa Tabora katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa huo Dakta Batilda Burihani amewataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi watumie siku moja  kima mwezi ku wa hamasisha wananchi kutumia vyakula bora,ili kujenga afya za wananchi wakulima kwa ujumla.