Back to top

Rwanda yafungua anga zake kwa safari za ndege za kimataifa.

01 August 2020
Share

Rwanda imefungua anga zake kwa safari za ndege za kimataifa, baada ya kusitishwa kwa kipindi cha siku 134, kutokana na tatizo la mlipuko wa virusi vya corona na safari ya kwanza ya shirika la ndege la Rwanda imefanyika leo ikiwabeba abiria kutoka Kigali kuelekea Dubai.

Mbali na Dubai shirika la ndege la Rwanda limerudisha safari zake za Dar es Salaa, Kilimanjaro, Douala, Kamembe Magaribi mwa Rwanda, Kigali, Libreville, Lusaka na Nairobi.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mkuu wa Shirika la Ndege la Rwanda  Bi.Yvonne Manzi, amesema ndege za Rwanda ni salama dhidi ya virusi vya corona kwani wamejipanga vilivyo ili kuhakikisha hakuna usambazaji wa corona unaotokea ndani ya ndege.


Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya taifa ya tiba Dr. Nsanzimana Sabin, amesema hawana wasiwasi juu ya kuenea zaidi kwa virusi vya corona nchini humo kufuatia kurejeshwa kwa safari za ndege za kimataifa.

Hayo yanajiri huku watu 28 wakiwa wamethibitika kuambukizwa virusi vya corona baada ya sampuli 3374 ya vipimo, kuchukuliwa katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita na sasa Rwanda imerikodi wagonjwa 2022.