Back to top

SAKATA LA MJAMZITO, ALEX ASIMAMISHWA KAZI KIGOMA

15 June 2024
Share

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, Bw.Fred Milanzi, amemsimamisha kazi Muuguzi wa Zahanati ya Basanza Bw.Alex Axsan Lyimo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za kutotekeleza majukumu yake ipasavyo, kufuatia video iliyomuonyesha mama mjamzito akijifungua kwenye zahanati hiyo bila msaada wa Muuguzi.

Bw.Milanzi amesema licha ya changamoto zilizojitokeza lakini mama huyo ambaye jina limehifadhiwa alijifungua salama na kupatiwa huduma zote zinazotakiwa na hatimaye kuruhusiwa kurudi nyumbani yeye na mwanae.

Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Nteghenjwa Hosseah ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, imesema Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Mohamed amesikitishwa na tukio hilo na kuwataka watumishi wa Afya kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia miiko ya taaluma zao.