Back to top

SAMWEL AMWAGIWA MAJI YA MOTO NA MPENZI WAKE

03 February 2023
Share

Rehema Prosper (41), mkazi wa Mtaa wa Bujingwa wilayani Ilemela mkoani Mwanza, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo, akituhumiwa kummwagia maji ya moto mgongoni, mpenzi wake, Timothy Samwel (33) kwa madai kuwa alikuwa akimsaliti kimapenzi na wanawake wengine.
.
Akitoa Taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Wilbroad Mutafungwa, amebainisha kuwa, Mtuhumiwa alifanya tukio hilo baada ya kumtembelea mpenzi wake na kupekua simu yake ya mkononi na kukuta mawasiliano mbalimbali na wanawake wengine ambao alikuwa akiwatuhumu kuwa wanatoka nae kimapenzi.