Back to top

SERIKALI KUENDELEA KUWEKEZA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE

09 February 2024
Share

Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt.Philip Mpango, amesema serikali ya Tanzania itaendelea kuwekeza zaidi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kutokana na Maendeleo makubwa ya afya na pia fedha nyingi za umma zimekuwa zikiokolewa na taasisi hiyo.

Makamu wa Rais amesema tafiti zinapaswa kufanyika kwa kina ili kubaini visababishi zaidi vya magonjwa ya moyo kwa kupata taarifa zaidi juu ya taratibu za kijamii na tabia za kiutamaduni katika mambo mbalimbali yaliyozoeleka kufanyika barani Afrika.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Magonjwa ya Moyo unaofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Airport Unguja, Zanzibar.

Amesema katika kukabiliana na ugonjwa wa moyo ni muhimu wananchi kufuata njia za kujikinga zaidi ikiwemo kuacha ulevi uliyopindukia, uvutaji sigara, tabia bwete pamoja na uzito uliyopindukia.