Back to top

Serikali kutoa magari 368 kwa Halmashauri 184.

28 December 2021
Share

Naibu Waziri TAMISEMI Dkt. Festo Dugange amesema serikali itatoa magari 368 kwa Halmashauri 184 nchini ambapo gari moja litakuwa la wagonjwa na gari jingine ni kwa ajili ya ufuatiliaji wa kazi za miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri na utoaji wa huduma za kijamii huku akibainisha kuwa ujenzi wa vituo vya afya kwa fedha za Tozo na fedha za Uviko -19 utaenda sambamba na ugawaji wa magari hayo.