Back to top

SERIKALI YAJITETEA GHARAMA ZIARA YA RUTO, MAREKANI

23 May 2024
Share

Serikali ya Kenya imetetea gharama zinazotumika kwenye safari ya Rais wa nchi hiyo William Ruto nchini Marekani, ambapo watu 30 akiwemo mcheshi maarufu nchini humo wameripotiwa kuandamana na Rais huyo kwenye ziara hiyo.
.
Kulingana na Kituo cha runinga cha KTN nchini Kenya, kimedai kuwa bei ya kukodisha ndege binafsi ya kifahari ambayo Rais Ruto na ujumbe wake wameitumia inakadiriwa kuwa Dola Milioni 1.5, huku Msemaji wa Serikali Bw.Isaac Mwaura akiwaambia waandishi wa habari kuwa faida za ziara hiyo ni kubwa mara milioni ya fedha hizo.
.
Rais Ruto yupo nchini Marekani kwa ziara ya siku nne kwa mwaliko wa Rais Joe Biden, na tayari wamekutana na kufanya mazungumzo katika ikulu ya Marekani iliyopo Washington DC. 
.
Baadhi ya raia wa Kenya, wameeleza kukasilishwa na maamuzi ya Serikali ya nchi hiyo kukodi ndege kutoka Kampuni ya RoyalJet inayomilikiwa na Dubai kwa ajili ya safari hiyo badala ya kutumia ndege yake ya kawaida ya Rais, huku wakidai kuwa haiendani na sera ya nchi hiyo ya kubana matumizi.