
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu amesema serikali imepeleka Shilingi bilioni 109 kwa ajili ya kujenga shule za sekondari 234 kwenye majimbo yote 214 nchini, huku akifafanua kuwa shule hizo ni miongoni mwa shule 1,000 ambazo zimepangwa kujengwa katika kata zisizo na shule za sekondari na zenye msongamano mkubwa wa wanafunzi kutokana na fedha za mkopo nafuu wa Shilingi trilioni 1.5.
