Back to top

Silinde:Watoto kukaa chini, kukosa madarasa, ni aibu na nifedhea.

22 July 2021
Share

Naibu Waziri ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde ameagiza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kutenga fedha katika mapato ya ndani wanayokusanya kuboresha sehemu za kazi za watumishi kwa kujenga nyumba za watumishi, madarasa na huduma zingine za halmashauri badala ya kutumia fedha hizo kwa vitu ambavyo haviwagusi wananchi moja kwa moja.

Kauli hiyo ameitoa baada ya kutembelea ujenzi wa nyumba sita za walimu ambazo zimejengwa na halmashauri ya manispaa ya Kahama mkoa wa Shinyanga katika shule ya msingi Tungulu ambayo walimu walikuwa wakiishi katika nyumba mbovu za udongo na kuchangia ufaulu mdogo wa wanafunzi shuleni hapo.

Aidha Naibu Waziri Silinde amesema ni aibu mpaka leo bado wanafunzi wanakaa chini au kwenye mawe darasani au kosomea chini ya miti kwa kukosa madarasa na kuagiza wakurugenzi ambao katika halmashauri zao kuna shida hizo watenge fedha kumaliza upungufu wa madawati na madarasa mapema iwezekanavyo.