Back to top

SIMULIZI ZISIZO NA uwepo wa USHIRIKINA MBIONI

16 June 2022
Share

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk.Doroth Gwajima, amesema Jamii inapandikiza mbegu isiyo nzuri kwa kuwahadithia watoto simulizi zisizo na afya kwa kuwasimulia mauaji ya wazee hali ambayo inajenga kizazi kisichokuwa na historia nzuri juu ya wazee hao.

Waziri Gwajima akiwa kijiji cha Kisharita, Iramba mkoani Singida, amefanikiwa kuzungumza na wazee na wanafuzi na kusema sasa Mabaraza ya wazee yataanza mpango wa kuzalisha hadithi za watoto zenye simulizi mpya zisizo na fikra za uwepo wa ushirikina na uchawi kwamba ni chanzo cha matatizo kwenye jamii.

Aidha Waziri Gwajima ameongeza kuwa katika juhudi za kupambana na ukatili kwa wazee, serikali imeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ikiwemo Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawane na Watoto.

Video ya Waziri Gwajima akiongea tumekuwekea kwenye Instagram yetu #ITVTANZANIA