
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mtwara imesema haitasita kushughulika na baadhi ya Wakurugenzi na Watendaji wa baadhi ya halmashauri watakaojaribu kwenda kinyume na maelekezo ya matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo ikiwemo shilingi Bilioni 11 zilizotokana na ugonjwa wa Corona zinazokwenda kwenye miradi ya Elimu, Afya na Maji.
.
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mtwara Enock Ngailo amesema hayo wakati akitoa taarifa ya kazi za ofisi hiyo ya kila miezi mtatu na kusisitiza kushughulika na wakurugenzi wakiwemo watendaji wa serikali wataokiuka maekezo ya fedha za miradi zilizoletwa na serikali kuu.
.
Amesema tayari ofisi ya TAKUKURU inamiongozo yote katika kusimamia matumzi ya fedha hizo katika miradi ya maendelo hivyo ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuwa sehemu ya kulinda fedha hizo zinazokwenda kwenye miradi ya elimu madarasa na maji.
.
Hata hivyo amesema TAKUKURU mkoa wa Mtwara imejipanga kutoa elimu maalum ili kuzuia ubadhirifu wa fedha katika miradi ya maendeleo.
