
Wizara ya TAMISEMI imesema imepata shilingi bilioni 6 kutokana na ushuru wa huduma za Mawasiliano na imeelekeza fedha hizo zikajenge nyumba 165 zitakazotumiwa na watumishi wa Elimu na Afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa TAMISEMI Mh.Ummy Mwalimu akiwa ziarani katika Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Mkoani Tabora, na kubainisha kuwa nyumba 54 zitakuwa ni 3 kwa 1; Yaan nyumba 1 itabeba familia 3 hivyo jumla itakua familia 162.
