Back to top

TANESCO: Kutakuwa na Upungufu wa Uzalishaji Umeme.

18 November 2021
Share

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limetoa taarifa kwa wateja wake kuwa kutakuwa na Upungufu wa uzalishaji wa umeme kwa takribani 345MW, ambayo ni sawa na 21% ya uzalishaji wote. Hali hiyo inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambapo viwango vya maji katika mito na mabwawa yanayotumika kuzalishia umeme ikiwemo vituo vya Kihansi, Kidatu na Pangani vimepungua.