
Katika kuelekea Mwaka mpya wa 2022 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne Muliro amesema jeshi hilo limeandaa vizuri mifumo ya kuzuia uhalifu kwa ushirikiano na wadau wengine wa masuala ya kiusalama.
"Sisi tumeshajipanga vizuri kuhakikisha kwamba hatutoi fursa kwa wahalifu, kwa maana hiyo katika mitaa, nyumba za ibada, nyumbani, ofisi mbalimbali za serikali na binafsi maeneo yote hayo sisi lazima tuhakikishe usalama unaimarika"-ACP Muliro Jumanne Muliro.
