Back to top

TUMEPIGA HATUA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI VVU-RAIS SAMIA

01 December 2023
Share

Ikiwa ni Siku ya Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema kama nchi tumepiga hatua katika kupunguza maambukizi mapya, lakini bado tunayo kazi kubwa ya kufanya kufikia lengo la kutokomeza kabisa maambukizi. 
.
Rais Samia ameyasema hayo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, ambapo amebainisha kuwa wanaendelea kushirikiana na wadau toka sekta binafsi na jamii kwa ujumla katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo, kwa kuzuia maambukizi mapya kwa makundi maalumu, hasa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24, hususan wasichana.