Back to top

"TUMUOMBEE RAIS SAMIA KATIKA KULIONGOZA TAIFA" - SILAA.

31 March 2024
Share

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Jerry Silaa amewataka waumini wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT) kuhakikisha wanamuombea Rais Samia Suluhu Hassan katika kazi yake ya kuliongoza taifa.

Silaa ameyasema hayo leo alipofungua harambee ya kuchangia upanuzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Chanika Jijini Dar es Salaam.

Katika hotuba yake mbele ya kanisa hilo, Waziri huyo amesisitiza umuhimu wa walutheri kumuombea Rais Samia.

Kauli yake hiyo inatokana na kile alichoeleza, Rais Samia akishiriki sherehe za kumsimika Mkuu wa KKKT, Dk Alex Malasusa, hatua ambayo inathibitisha upendo wa Mkuu huyo wa nchi kwa waumini wa kanisa hilo.

Hata hivyo, Silaa amekabidhi jukumu hilo la maombi kwa Mkuu wa KKKT, Dk Malasusa akisema anapaswa kuhakikisha waumini wote wanamuombea Rais Samia.