Back to top

Uchaguzi mpya wa Urais Malawi Kufanyika Julai 02, 2020.

24 March 2020
Share

Tume ya Uchaguzi nchini Malawi imetangaza kuwa uchaguzi mpya wa Urais nchini humo utafanyika Julai 02, 2020 baada ya Mahakama kufuta uchaguzi wa Mei 2019 uliompa ushindi Rais Peter Mutharika.

Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Katiba Healey Potani amesema mahakama hiyo iliyafuta matokeo ya uchaguzi huo kutokana na dosari nyingi zilizoufanya usiwe huru, haki na wa kuaminika.

Mahakama hiyo imeitaka Tume ya uchaguzi isitishe kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Mei 21 kwa sababu ya madai ya udanganyifu.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Mei 21 mwaka 2019, Tume ya Uchaguzi ilimtangaza Bwana Peter Mutharika kuwa mshindi kwa kupata asilimia 38.6 ya kura zote.