Back to top

Ufaransa kukarabati Uwanja wa Ndege “Terminal Two”.

19 October 2021
Share

Tanzania na Ufaransa zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika maeneo ya kimkakati ikiwemo Nishati, Elimu, Kilimo na Miundombinu ambapo Ufaransa umekubali kukarabati Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ‘Terminal Two’ Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameyasema hayo wakati akizungumza na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester leo alipowasili Jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya siku moja.   

Kumekuwa na Miradi ambayo Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lao la Maendeleo wamekuwa wakifadhili Miradi mbalimbali katika Sekta 
Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester yupo nchini Tanzania kuzindua safari za Shirika la ndege la Ufaransa ‘Fance Airline’ kutoka Paris hadi Zanzibar ambapo mara ya mwisho kwa shirika hilo kufanya safari zake hapa nchini ilikuwa mwaka 1974.

Septemba 15, 2021 Balozi wa Ufaransa hapa nchini Mhe. Nabil Hajlaouvi alisema Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lake la ndege ‘Fance Airline’ inategemea kuanzisha safari mpya ya ndege kutoka Ufaransa moja kwa moja hadi Zanzibar kuanzia 19 Oktoba 2021.