
Wanafunzi waliohitimu masomo katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto Tanzania kilichopo Handeni mkoani Tanga wamesema Chuo hicho kinakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa ya kujifunzia na uhaba wa maji hali inayopelekea masomo ya darasani kuendeshwa kwenye Ukumbi wa mikutano wa chuo uliopo sasa ambao hautoshelezi mahitaji.
