Back to top

Uingereza yakiri matukio ya udukuzi kuwa tishio siku za usoni.

16 October 2018
Share

Uingereza imesema haina mashaka sana na matukio ya udukuzi wa kimtandao yanayoikumba nchi hiyo mpaka sasa ingawa inakiri kuwa huenda katika siku za usoni matukio hayo yakawa tishio la usalama nchini humo.

Afisa Mtendaji mkuu wa kituo cha Taifa cha usimamizi wa masuala ya usalama wa mtandao nchini Uingereza (NCSC) Ciaran Martin anasema kuwa  kuna wastani wa mashambulizi 10 ya kimtandao kwa wiki na wamejitahidi kuyadhibiti yasifanye athari zozote na kwamba kwa kipindi cha miaka miwili tangu kuanzishwa kwa kituo hicho wameweza kupambana na matukio 1,167 yakiwemo  557 yaliyotokea ndani ya miezi 12.

Amesema mashambulizi hayo ya kimtandao mengi wamegundua yaliendeshwa na makundi ya wadukuzi wa kompyuta wanaoonekana kufadhiliwa na serikali za nchi yaliyopo makundi hayo.

Ciaran Martin anakiri kuwa vitendo vya makundi hayo vinatishia usalama wa taifa wa Uingereza.