Back to top

UJENZI WA IKULU YA CHAMWINO WAFIKIA 91%

16 January 2022
Share

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ikulu inayojengwa katika eneo la Chamwino, Jijini Dodoma na kusema kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi na ubora wa majengo ambao umefikia asilimia 91% huku 9% zilizobaki zikiwa ni kazi ndogondogo kama uwekaji wa milango, njia za mifumo ya hewa na umeme na zote zinaenda vizuri ambapo amemtaka mkandarasi ahakikishe mradi huo unakamilika mwezi Mei mwaka huu.