
Zaidi ya mifugo elfu hamsini inadaiwa kufa kutokana na kukosa malisho pamoja na maji kwenye mikoa ya kanda ya kaskazini huku wafugaji kutoka katika mikoa minne ya kanda hiyo wakilazimika kuhamishia mifugo yao katika kijiji cha Karambandea kilichopo wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro ambako kunatajwa kuwa na maji ya kunyweshea mifugo.
