
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera inakabiliwa na upungufu mkubwa wa damu kwa ajili ya wagonjwa wanaoihitaji hasa wanaopata ajali za barabarani, wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
.
Ili kukabiliana na upungufu huo, Mshauri wa Kitengo cha Damu Salama katika hospitali hiyo Amos Bashweka amewaomba wananchi wajitolee damu ili kunusu uhai wa wanaoihitaji kwani mahitaji ya damu salama katika hospitali hiyo kwa mwezi ni kati ya chupa 180 na 250.
.
Katika kuunga mkono ombi hilo, wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Halotel ambao wameojitokeza kutoa damu, wameahidi kufanya hivyo mara kwa mara kwa ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
