Back to top

Utafiti waondoa utata kuhusu mahali alipotokea mwanadamu wa kwanza.

05 May 2018
Share

Hatimaye utata uliokuwa ukiendelea duniani kwa watafiti wa mambo ya kale kuhusiana na mahali mwanadamu wa kwanza alipotokea umemalizika baada ya jopo la wataalam liloundwa na Wizara ya Maliasili na utalii kufuatia ushahidi wa vinasaba kubaini kuwa binadamu huyo alitokea barani Afrika huku ikidaiwa kuwa ni Tanzania.

Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Mhe Japhet Hasunga ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha wadau wa mazao ya nyuki amesema kuwa utafiti huo umeshirikisha wataalamu kutoka mataifa mbalimbali duniani ambapo amesema kuwa kumalizika kwa utafiti huo utaiwezesha nchi kukua katika sekta ya utalii na kuchochea uchumi wa nchi.

Akizungumza kwa njia ya simu Mkurugenzi mkuu wa Makumbusho ya taifa Prof. Audax Mabula ambaye alikuwa kiongozi wa jopo la utafiti amesema utafiti huo ulifanywa kwa lengo la kuondoa utata uliokuwa ukiendelea duniani ambapo amesema kuwa bado wanaendelea na tafiti mbalimbali zitakazowezesha kukuza sekta ya utalii.

Baadhi ya wakazi mkoani Dodoma wamesema kuwa kufuatia utafiti huo utawezesha Tanzania kupata watalii wengi kutoka mataifa mbalimbali duniani ambapo wameiomba serikali kupitia makuymbusho ya taifa kutangaza utafiti huo kama chachu ya kukuza sekta ya utalii hapa nchini.