Back to top

Vifo vya watoto wachanga bado ni tatizo Arusha.

23 April 2018
Share

Tatizo la watoto wachanga kupoteza maisha bado ni kubwa katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Arusha ambapo wataalamu wa afya wanasema katika wilaya ya Arusha pekee watoto zaidi ya 200 hupoteza maisha kila mwezi.

Mganga mkuu wa jiji la Arusha Bi.Jeni Balalikwiliza amesema tatizo hilo linachangiwa na uhaba wa vifaa tiba katika hosipita na vituo vya afya hasa vilivyoko pembezoni na kwamba wanaendelea kulikabili kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali.

Katibu tawala wa wilaya ya Arusha Bw. David Mwakiposa amesema tatizo hilo linaendelea kupungua baada ya vituo nane 8 vya afya kupatiwa vifaa tiba vya kisasa.

Baadhi ya wananchi pamoja na kupongeza jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya sekta za afya wameiomba kuongeza nguvu katika upatikanaji wa vifaa tiba kwani bado ni tatizo hasa katika hosipitali na vituo vya afya vilivyoko pembezoni.