
#HABARI: Watoto wawili wa familia moja katika kijiji cha Mwabagaru kata ya Buseresere wilayani Chato mkoani Geita wamefariki dunia huku wengine watatu akiwemo mama yao mzazi wakilazwa katika Kituo Cha Afya Bwanga baada ya mama yao mzazi kuwanywesha sumu ya kuulia wadudu wa mazao kwa madai ya ugumu wa maisha.
