Wananchi wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wanaendelea kusumbuliwa na Tembo wanaoharibu mazao yao na kusababisha vifo ambapo kutokana na changamoto hizo baadhi yao wameanza kuwaita waganga wa jadi kusaidia kuzuia na kuwafukuza tembo mashambani kwa njia za kishirikina.
Kutokana na changamoto hizo shirika la uhifadhi wa maliasili na mazingira la Pams Foundation limetoa semina elekezi kwa wananchi juu ya teknolojia ya kufukuza Tembo kwa kutumia pilipili,oil chafu na kuchoma tofali la pili pili
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Tunduru Bw. Julius Mtatiro amewataka wananchi kuacha kuamini kwamba Tembo anaweza kuzuiwa kwa kutumia ushirikina