
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa amewataka Wakandarasi wanaojenga Daraja la JPM Kigongo-Busisi kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa huku akisisitiza kuwa Daraja hilo lizalishe vijana wengine wa Kitanzania wenye uwezo wa kujenga madaraja hapa nchini.
