Back to top

Wakuu wa Mikoa watakiwa kutunza na kuhifadhi maeneo ya Kihistoria.

27 February 2021
Share

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa nchini kutunza na kuhifadhi maeneo ya kihistoria huku akisema makumbusho ya vita vya majimaji yaliyopo Songea mkoani Ruvuma ni kielelezo cha ushujaa wa Watanzania.

Ametoa maagizo hayo kupitia hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe.Innocent Bashungwa wakati akizungumza kwenye kumbukizi ya miaka 114 ya vita vya majimaji mjini Songea.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa makumbusho ya taifa Dkt.Noel Lwoga amesema makumbusho ya vita vya majimaji imebeba historia kubwa ya mwafrika na uzale0ndo na kujiamini.

Katika kumbukizi hiyo wadau wa makumbusho kutoka chama cha urafiki baina ya Songea na Ujerumani Dkt.Xaver Kazimoto Komba amekuwa na haya ya kusema kuhusiana nakudumisha mahusiano mema baina ya Tanzania na Ujerumani nchi ambayo ilikuwa mkoloni wa Tanganika.