Back to top

WALIOHUSIKA KUPOKEA WAFUGAJI KIHOLELA KUCHUKULIWA HATUA MKURANGA.

03 November 2021
Share

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Abdallah Ulega amemtaka mkuu wa wilaya ya Mkuranga Khadija Nasiri kuhakikisha anachukua hatua za kisheria kwa wote waliohusika na kuwapokea wafugaji kiholela bila kufuata utaratibu na kusababisha migogoro wilayani humo.
.
Ulega ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya wafugaji na wakulima aliyofanya katika kijiji cha Dondo halmashauri ya wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Khadija Nasiri amesema kufuatia uvamizi wa wafugaji wameshaanza kuchukua hatua mbalimbali ili kudhibiti hali hiyo.
.
Awali wakulima wanaofanya shughuli zao katika wilaya hiyo katika nyakati tofauti wamesema wafugaji wamewasababishia madhara makubwa ikiwemo kuliwa mashamba yao na kuwatishia pale wanapotaka kudai haki zao.