Back to top

Wanafunzi wa kike Arumeru waomba wazazi wasaliti kuchukuliwa hatua.

15 June 2019
Share

Wanafunzi  wa kike wa shule za msingi kutoka vijiji vya wilaya ya Arumeru wameiomba serikali ianze kuchukua hatua kali kwa wazazi  wa wilaya hiyo ambao wanaungana na watu wanaowapatia ujauzito watoto wa kike kwa kuzungumza na kuyamaliza kienyeji baada ya kupatiwa fedha hali inayowaathiri kisaikolojia na kukatisha ndoto zao katika masomo.


Wanafunzi hao wakike wametoa kauli hiyo katika kusanyiko lililowakutanisha wanafunzi wazazi viongozi wa madhehebu ya dini na watendaji wa serikali wilaya ya arumeru kuelekea maazimisho ya siku ya  mtoto wa afrika ndipo wakapata nafasi ya kufikisha kilio chao kwa serikali na wadau wa elimu.


Viongozi wa madhehebu ya dini wanasema wanaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa mpango wake wa elimu bure kwani umewezesha kuokoa watoto wengi waliyokuwa wanaingia mitaani baada ya wazazi wao kukosa uwezo wa kugharimia masomo.