Back to top

Wanafunzi wapumzike wakati wa likizo - Ummy.

27 November 2021
Share

Waziri wa TAMISEMI Mh. Ummy Mwalimu amewaagiza wakuu wa Mikoa na Wilaya zote nchini kuhakikisha wanasimamia suala la wanafunzi kupumzika wakati wa likizo ili kuwapatia watoto muda wa kujifunza masuala mengine ya Kijamii. 
.
Waziri Ummy ametoa agizo hilo baada ya kupata maelekezo ya kisera kutoka kwa Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako ambaye amemtaka kulisisitiza suala hilo ili wanafunzi waweze kupata muda wa kupumzika kipindi cha likizo.