Back to top

Wananchi walalamikia wafanyakazi TANESCO kunena lugha za matusi

08 December 2019
Share

Baadhi ya wananchi na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, wamewalalamikia wafanyakazi wa shirika la ugavi wa umeme nchini TANESCO wilayani humo, kutoa lugha za matusi kama sehemu ya kupandisha munkari ya kufanya kazi wakati wa kusimika nguzo za umeme na kwamba hali hiyo inaharibu maadili katika jamii.
 
 
Baadhi ya wananchi hao katika wilaya ya nyasa mkoani Ruvuma, wamesema kitendo cha wafanyakazi wa TANESCO wilayani humo kunena lugha za matusi kwa madai ndiyo munkari ya kufanya kazi wakati wa kusimika nguzo na kuvuta nyaya za umeme kimekithiri mno na kwamba inaharibu maadili kwa jamii.
 
Malalamiko hayo yakatinga katika kikao hiki cha baraza la madiwani wilayani Nyasa, huku kubwa madiwani wakihoji mahusiano ya kunena lugha za matusi na kazi hiyo.
 
Meneja wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO), wilaya ya Nyasa, Bw. Kanuti Runguti, anasema shirika lilishapiga marufuku wafanyakazi wote kunena lugha za matusi wakati wa kazi na kwamba atafuatilia malalamiko hayo.