
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.George Simbachawene ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kufanya msako mkali wa kuwabaini watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria, Mhe. Simbachawene ametoa agizo hilo kufuatia kumalizika kwa muda wa kusalimisha silaha hizo huku akibainisha kuwa asilimia kubwa ya silaha zilizosalimishwa ni silaha za kienyeji hususani magobore.
