
Wanaume mkoani Ruvuma wametakiwa kuacha kuvumilia vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa na wake zao ikiwemo kupigwa na badala yake watafute usuluhishi ili kuepuka kutokea kwa madhara makubwa ikiwemo mauaji.
.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Dawati la Jinsia mkoani humo, Insepkta Odilia Mrosso, katika uzinduzi wa Wiki ya Sheria.