Back to top

WATAALAM WA KUJENGA BWAWA WAWASILI ARUSHA

19 April 2024
Share

Jopo la Wataalam kutoka Wizara ya Maji limewasili Nanja ,wilayani Monduli ,mkoa wa Arusha, tayari kwa kuanza kazi  ya kujenga bwawa lililobomolewa na maji .

Waziri wa Maji Mh Jumaa Aweso, ambaye amepiga kambi kwa muda katika eneo hilo, amesema wataalam hao watakaa katika eneo hilo hadi kazi itakapokamika.

Mkuu wa Wilaya ya Monduli  Bw Festo Kiswaga, amesema pia Jeshi la Wananchi wa Tanzania,  limetoa msaada maligafi kama vile mawe na mchanga,  kwa ajili ya kuharakisha ujenzi wa bwawa hilo.

Mbunge wa wilaya ya Monduli Mh, Fredrick Lowassa, ameishukuru serikali kwa kuchukua hatua hiyo, na amewataka wananchi wa Nanja kwa ujumla  kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa hali na mali kwa wataalam hao .