
Watu 7 kati 14 waliokuwa wakisafirisha magunia ya mpunga kwa kutumia mtumbwi katika bonde dogo la Kitongoji cha Lunguya, Kijiji cha Mwamapuli kilichopo Halmashauri ya Mlele, mkoani Katavi, wamepoteza maisha baada ya mtumbwi huo kupinduka.

Akizungumza na ITV, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Katavi, Inspekta Lilian Wanna, amesema tukio hilo lilitokea Mei 24, 2024 majira ya saa kumi na mbili jioni na kwamba wanaendelea na juhudi za uokoaji licha ya kuwa bonde hilo lina changamoto ya mamba na viboko.
.
Inspekta Wanna amesema watu hao walikuwa wakitoa mazao yao shambani na kuyapeleka Kijijini wakati ajali hiyo inawakuta.
.
Bw.Nuhu Bahati ambaye amepoteza ndugu zake wawili akiwemo mtoto wa miaka 14, ameiambia ITV kuwa ndugu zake walimuacha kambini kwa lengo la kuwahi kuchaji simu zao.
