Back to top

WATU KUNYONGWA, BALOZI IRAN KUHOJIWA

17 January 2023
Share

Balozi wa Iran nchini Ujerumani ameitwa kuhojiwa kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha wiki moja na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, kuhusiana na wimbi la kunyongwa watu kadhaa na serikali ya Iran na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Msemaji wa Baerbock, Christopher Burger amethibitisha kuhusu hatua hiyo baada ya kuulizwa kuhusu kuhojiwa kwa balozi Mahmoud Farrazandeh.

Nchi mbali mbali za Magharibi na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu wamelaani ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Iran kufuatia kunyongwa kwa watu kadhaa waliokuwa wakizuiliwa jela.

Jumamosi Iran imesema imemnyonga raia wake mmoja mwenye uraia pia wa Uingereza aliyehukumiwa kifo kwa kuendesha ujasusi nchini Iran kwa niaba ya Uingereza.