
Watu wanne katika kijiji cha Namasalau kata ya Tuwemacho wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wamefariki dunia kwa kuugua ugonjwa wa ajabu wa kukohoa na kutapika damu huku wananchi wakiuhusisha ugonjwa huo na ushrikina.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Bw. Juma Homera ametembelea kijiji hicho kujionea hali halisi na amesema serikali imechunguza ugonjwa huo na bado haujabainika ni ugonjwa gani na kwamba uchunguzi bado unaendelea huku wananchi wakitaka awaletee awaletee mganga wa kienyeji.
