Baraza la madiwani la halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni limewafukuza kazi watumishi watatu mhandisi , daktari na muuguzi wa halmashauri hiyo baada ya kubainika kugushi vyeti vya uhandisi na kidato cha nne.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi Bw. Ally Minja amesema hayo kwenye baraza la madiwani la halmashauri kuwa watumishi hao walifukuzwa kazi baada ya kusimamishwa kwa muda mrefu na baada ya baraza kuridhika limepitisha uamuzi huo.