
Watu wawili wamefariki huku wengine wawili wakijeruhiwa kufuatia ajali ya ndege ya Shirika la Frankfurt Zoological aina ya Cessna 182 yenya namba za usajili 5H-FZS, iliyoanguka muda mfupi baada ya kuruka kwenye kiwanja kidogo cha ndege cha Matambwe, Selous.
.
Timu ya uchunguzi wa ajali kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) imeshaanza uchunguzi kujua chanzo cha ajali hiyo na itatoa taarifa kwa mujibu wa sheria.

