Back to top

Waziri Dkt Mabula amkabidhi tuzo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

03 July 2022
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amemkabidhi Rais Mstaafu wa serikali ya awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete tuzo aliyokabidhiwa wakati wa Mkutano wa tisa wa Viongozi wa Majiji uliofanyika mwishoni mwa mwezi Mei 2022 huko Kisumu nchini Kenya.

Tuzo aliyokabidhiwa Kikwete ni tuzo ya heshima iliyotolewa na Taasisi ya United Cities and Local Government of Africa (UCLG Africa) ikiwa ni kutambua juhudi zake za kuimarisha Mamlaka ya Serikali za Mitaa (Commitment in Fevour of the African Movement of the Territorial Government)

Dkt Mabula amemkabidhi Tuzo hiyo mkoani Arusha mara baada ya halfa ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mfuko wa Wanyamapori Afrika (AWF) yaliyofanyika Julai 1, 2022 katika Kituo cha Urithi wa Utamaduni.

Wakati wa mkutano wa majiji maarufu kama Africities uliobeba kauli mbiu ya mchango wa miji inavyoweza kuchangia utekelezwaji wa dira ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 na Umoja wa Afrika mwaka 2063 mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo hali ya miundo mbinu kwenye miji na namna bora ya kuimarisha maisha ya wakazi wa miji hiyo.