Back to top

WAZIRI MABULA ATAKA WANASIASA KUWA WAKWELI

09 May 2022
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula amewataka wanasiasa nchini kuwa wakweli wakati wa kutekeleza  majukumu yao ili kuepuka kuleta migongano baina ya serikali na wananchi.

Dkt.Mabula ametoa kauli hiyo mkoani Mbeya wakati kamati ya Mawaziri wa wizara za Kisekta walipokutana na uongozi wa mkoa na wilaya kwa lengo la kutoa mrejesho wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.

"Tusitafute kura kwa kudanganya wananchi halafu mwisho wa siku tunakosa maneno mazuri ya kuwaambia kwa sababu uliwaaminisha wakati ukiwa kiongozi na utakuwa na kugugumizi cha kwamba  utaenda kusema nini wakati uliwaaminisha"Amesema Dkt.Mabula

Waziri Dkt Mabula aliwataka wanasiasa kuwa wakweli kwenye mambo ambayo ni kwa ajili ya ulinzi, maendeleo na mustakabali wa nchi na kama walikosea huko nyuma basi wajisahihishe  na wasione aibu kuzungumza kama kuna makosa yalifanyika.