Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa amemwakilisha Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa njia ya mtandao kwenye Mkutano wa Jukwaa la Nne la Vijana Duniani lililoanza leo jijini Sharm-El-Sheikh, Misri ambapo ameyaomba mataifa makubwa duniani yashirikiane na nchi za Afrika ikiwemo Tanzania ili kuhakikisha uchumi wa nchi hizo unarejea katika hali yake ya kawaida kutokana na madhara ya UVIKO-19.