Back to top

Waziri Mkuu Majaliwa aongeza siku 7 uchunguzi chanzo cha moto Kariakoo

21 July 2021
Share

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema ameongeza siku 7 zingine kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha moto soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam, ulioteketeza soko hilo na mali za wafanyabiashara.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema amelazimika kuiongezea tume hiyo ya uchunguzi hadi tarehe 25 julai mwaka huu, ili tume hii iweze kubaini kiini cha tatizo hilo kabla ya mambo mengine kuendelea.